Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Naseeb Abdul "Diamond Platnumz " Simba , Ruge Mutahaba wa Clouds Fm na wengine wengi wakishiriki Kampeni ya Usafi Leo Dar ya Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiongoza maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika matembezi maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi katika jiji hili #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu. Karume, Ilala na kuishia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.
“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.
“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda.
Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.
Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.
Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.
2 comments:
Wakati mwingine inatubisi waBongo tuwe na ubunifu wa ziada. Yaani hapa inaonekana usanifu mtupu? Nasema hivyo kwa maana gani? Hiki ni kipindi cha masika na mvua nyingi zimekuwa zikiendelea kunyesa jijini, na kwa uzoefu mkubwa wa jiji la dar tokana na miundo mbinu mibovu kupindukia mafuriko yanasambaa hadi kwenye barabari maarufu za jiji.
Sasa wahusika hapo kwenye picha mkiongozwa na Mkuu wa Mkoa Paul, mmetubebea mifagio kwa kutuonyesha kuwa mnaenda kufajia maji au kuzibua mitaro ya maji na ile ya pembezoni mwa barabara ambako kunajaa taka na kuziba kila matoleo ya maji kusambaa kwenda baharini!! Ni vyema hata mngelituonyesha mkikusanya taka au kusafisha mifereji ya kusambaza maji tungelielewa kuwa kuna kazi inafanyika hapo. Kusema ukweli huu ni usanii mtupu na sidhani kama tutaendelea kufanya hivi tutafika mbali na kuliweka jiji letu safi ipasavyo. Tusipende Zaidi kuonekana mitandaoni na kwenye magazeti! tuwajibike ipasavyo kwa ajili ya wapiga kura!.
Usafi hauna masika wala kiangazi sisi watanzania ni watu wa ajabu sana siku zote tupo katika kurejeshana nyuma kila tunapoona mwenzetu anania ya kufanya jambo la maana. Yaani ni watu wa hovyo sana vipi mtu mwenye akili zake atakwenda kuwazodoa watu wenye nia safi kabisa ya kuhimiza usafi hasa wakati huu wa masika ambao kila mtu anaelewa wakati kama huu mara nyingi ndipo maradhi ya mripuko kama kipindupindu na kadhalika ni season yake kutokana na kutoweka mazingira safi. Tunajijua watanzania ni wanafiki lakini linapokuja suala la afya na maisha ya watu lazima tuwe wakweli Makonda na wale wote mlio katika kampeni ya kuhakikisha Daresalam inakuwa salama kwa usafi hongereni sana kwani nyinyi ni watu wa mfano.
Post a Comment