ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 15, 2016

RAIS WA SUDANI YA KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI.

Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) ambayo ilimbeba Rais wa Sudani ya Kusini, Mhe. Jeneral Salva Kiir Mayardit ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (mwenye tai nyekundu) akielekea kumpokea Rais wa Sudani ya Kusini, Mhe. Jeneral Salva Kiir Mayardit baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

No comments: