Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014
iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.
TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma
kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na
Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu
Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa
huru.
Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu
wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama
ya juu.
No comments:
Post a Comment