ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 18, 2016

UPDATE - TAARIFA YA AJALI YA KAKA ANDREW SANGA

Hali ya ndugu yetu Andrew Sanga (Drew) aliyepata ajali jana bado siyo nzuri na yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Prosper Kiswaga madaktari wanategemea kumfanyia uchunguzi mwingine asubuhi hii ya leo kabla ya kutoa taarifa ya nini watakachokifanya kuhusiana na hali ya mgonjwa. Mgonjwa bado yuko katika hospitali ya Memorial Hermann Southwest, 7600 Beechnut St, Houston, TX 77074
Kwa mujibu wa Bw. Kiswaga, madaktari wanashauri kusiwe na mkusanyiko mkubwa wa watu hospitalini hapo hadi hali ya ndugu yetu Andrew itakapotengamaa.

Taarifa zaidi zitawajia kila zitakapopatikana

Ahsanteni

Cassius Pambamaji
Msemaji wa THC

2 comments:

Ny Ebra!!!!!! said...

God of miracles come we need your supernatural love to break through nothing impossible your the God of miracles.

Anonymous said...

Jamani jamani jamani .maskini Andrew .Andrew Mungu akupiganie maana Zoe mwanao .Emmy be strong