Hali hiyo ilitokea jana bungeni mjini hapa, baada ya baadhi ya wabunge wa CCM kuwapiga vijembe wenzao wanaotoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutokana na kumteua kuwa mgombea urais na kumuunga mkono katika Uuhaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo, kutajwa kwa Lowassa ndani ya bunge na kuibua mjadala, nusura kusababishe vurugu hivyo kumlazimu spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha kikao mpaka jana jioni.
Vienne hivyo viliibuliwa na Mbunge wa Madaba (CCM), Joseph Mhagama, alipokuwa akichangia Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2015/16 hadi 2020/21.
Mbunge huyo alisema uchumi wa Tanzania utaimarika ikiwa serikali itawekeza kikamilifu katika viwanda, lakini akajikuta anatoka kwenye hoja na kuanza kuwashambulia wapinzani akidai wanapinga utaratibu wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kutumbua majipu.
Mhagama alisema anawashangaa wapinzani kwa kuwa vigeugeu, akidai wanawaunga mkono mafisadi ilhali kipindi cha nyuma sera kuu ya upinzani ilikuwa kupambana na ufisadi.
Wakati akiendelea kuchangia, Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, alisimama na kuomba kutoa taarifa ambayo alieleza kuwa upinzani haupingi utumbuaji majipu.
Heche alisema upinzani unaunga mkopo utaratibu huo na kufafanua kuwa hata sababu za kutumbuliwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, ziliwahi kuelezwa bungeni na aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje.
Heche alikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa majipu yanayotumbuliwa yalitengenezwa na CCM na kwamba Mhagama ni sehemu ya majipu hayo.
Baada ya taarifa hiyo, Mhagama alikataa kuipokea baada ya kuuulizwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, akisisitiza kuwa hawezi kupokea taarifa ya wapinzani ambao walileta taarifa bungeni kuwa Lowassa ni fisadi, lakini wakampitisha kugombea urais.
Siwezi kuipokea taarifa hiyo kwa sababu wapinzani hawa hawa walioleta taarifa hapa bungeni na kutuaminisha Lowassa ni fisadi, mwaka jana walimkumbatia na kumpa nafasi ya kugombea urais,alisema Mhagama, huku wabunge wa CCM wakishangilia kwa kupiga makofi.
Baada ya kuona hali inaelekea kuchafuka bungeni, Spika (Ndugai) aliasitisha kikao hicho cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 hadi saa 11:00 jioni.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni, naye aliwapiga vijembe wapinzani wakati akichangia mpango huo akieleza kufurahishwa na uamuzi wa kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge hilo. Chegeni alidai kuwa wapinzani sasa hawana ujanja kutokana na kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. "Hata vijembe hapa bungeni sasa vimepungua kwa sababu hakuna anayeona kule. Tujengane hapa kwa hoja na si mbwembwe ambazo hazina faida kwa wananchi," alisema.
Source: Jicho1 Blog
Our opposition is truly beginning to disappoint me. this is a group that relentlessly claimed Hon. Lowassa was a corrupt CCM leader: a poster child of corruption in Tanzania. Suddenly, when CCM dumped him it quickly turned to him to lead it during the 2015 elections as its candidate! I was indeed disappointed. However, Tanzanians knew better and spoke, and now the rest is history.
ReplyDeleteAs one who supports a credible opposition, I cannot understand why the opposition is so indebted to Lowassa and continue to find merit in defending him so fervently! Isn't there a more credible alternative in their ranks? It is saddening. Poor Tanzania.
Bunge na waTanzania wenye mapenzi mema na nchi yao wanatakiwa kuelewa somo. Hili swala la kusema Lowassa fisadi halikuanza leo na badala yake yote anayofanya ni mema kwa waTanzania na vizazi vyenye mahitaji ya mabadiliko na maendeleo.
ReplyDeleteMafisadi lukuki wako CCM wanaendelea kutesa na hao waliokamatwa wachache na kudaiwa kufunguliwa mashtaka mahakama inapoanza rasmi. Kwa mtizamo yakinifu sioni umuhimu wa kuibua hoja ya Lowasa ambayo haina kichwa na kama kipo basi kinamhusu kiongozi wake mkuu aliyekuwepo madarakani nadhani vyema aanzwe yeye. Vinginevyo wabunge fanyeni kazi mliyopewa na waTanzania na acheni ukiukwaji wa kazi mliyotumwa.
Mafisadi mnawajua waondoeni huko mlikowaficha na LUGUMI msije kuua hoja hii muhimu.