ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 4, 2016

MADAM SOPHY CHARITY MOVEMENT NA TANZANIA ACTION FOR DISABLED WATOA MSAADA WA VITABU VYA HISABATI KWA SHULE YA SEKONDARI YA TURIANI

Taasisi ya kijamii yenye malengo ya kusaidia walio na mahitaji maalum ijulikanayo kama Madam Sophy Charity Movement kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Action for Disabled zote zimegawa vitabu vya hisabati vilitolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Action for Disabled kwa shule ya Sekondari ya Turiani iliyopo Magomeni jijini Dar Es Salaam, Madam Sophy amabye ni muasisi wa Madam Sophy Charity Movement akishukuru kwa waliofika kwa ajili ya tukio hilo hasa muwakilishi wa Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Halima kwa kujuika na wadau walioweza kufika katika hilo.

Taasisi hii iliyoanzishwa hivi karibuni inandelea na huduma zake za kusaidia watoto walio na mahitaji maalum na walemavu imeweza kukusanya wadau ambao pia ni wajumbe wa Madam Sophy Charity Movement wanaojitolea pesa hata mali kwa ajili ya jambo hili.
Mc Manyama akizungumza na wanafunzi mapema leo kabla ya tukio la kugawa vitabu kuanza nae aligawa zawadi kwa mwanafunzi aliyehiari kufanya chochote mbele ya wenzake.
Mc Manyama akizungumza na wanafunzi mapema leo kabla ya tukio la kugawa vitabu kuanza nae aligawa zawadi kwa mwanafunzi aliyehiari kufanya chochote mbele ya wenzake.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani Mwalimu Beatrice Mhina akitoa utambulisho kwa ugeni wake ulitembelea katika shule na kulia ni Madam Sophy ambaye ni muasisi na mwanzilishi wa Madam Sophy Charity Movement.
Muwakilishi wa Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Halima Sangali alisimama na kujitambulisha huku akipongeza jitihada za Madam Sophy kwa kusaidia wahitaji walio walemavu na wenye mahitaji maalum, huku akitoa msisitizo kutowatenga walio na ulemavu kwani ni ndugu wa jamii zetu.
Muwakilishi toka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Action for Disabled Bi Frola Furaha Mwakasege yenye makao yake makuu nchini Uingereza na Tawi lake jijini Dar Es Salaam maeneo ya Posta, ambao pia ni wafadhili wa vitabu vya hisabati kwa ajili ya kugawa kwa watoto wenye mahitaji maalum,"..leo tumeweza kuleta vitabu vya hisabati kwa ajili ya kuvitumia pia naamini mtafanya vizuri katika somo hilo na mengine pia" alisema Bi Frola 
Madam Sophy ambaye ni muasisi na mwanzilishi wa Madam Sophy Charity Movement akijitambulisha na kutambulisha wadau wa Madam Sophy Charity Movement(ambao hawapo pichani) "Sisi ni vijana na kwa umri tulionao tunaweza kufanya mazuri tena makubwa sio lazima kuyafanya tukiwa matajiri, maadamu tu wazima tunaweza kusaida wenzetu wenye ulemavu" Madam Sophy alisema. Pia kwa mwezi wa Julai kumetarajiwa kuwa na uzinduzi wa Madam Sophy Awareness Club ambayo pia itahusika kuhamasisha vijana hususani wanafunzi ikilenga kundi hilo wapate kujitambua, kujipenda, kujithamini na kujiamini pia.
Picha ya pamoja ilipigwa pia 

No comments: