ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 3, 2016

Makonda Atoa Siku 7 Kumaliza Watumishi Hewa

1 comment:

Unknown said...

Hongera sana, kijana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa suala hili la watumishi hewa!
Ninakupongeza lakini ninasikitika ya kuwa mijadala ya watumishi hewa imeendelea kujadili watumishi bila kusema chochote kwa hawa waajiri ambao kwa mjibu wa sheria walifanya uzembe mkubwa saaana wa kuwalipa watu ambao wanafahamu hawafanyi kazi. Mimi ninafahamu ya kuwa, ukitaka kufahamu watumishi hewa, chukua nyaraka za orodha ya malipo kutoka Wizara ya Fedha yaani payroll alafu chukua taarifa ya malipo yaani 'Payment Vouchers'za mwezi husika alafu nenda Benk uangalie kiasi gani cha fedha kilipelekwa na waajiri kama malipo. Hapo utaona ya kuwa fedha iliyopokelewa kama fedha ya malipo hewa imekwenda wapi.
Kiutaratibu, payroll zikifika kutoka Hazina, Mkurugenzi, Mweka Hazina(kitengo cha mishahara) uchambua na kuondoa watu ambao hawastahili kulipwa mishahara then uandaa maelekezo kwenda Bank kwa ajili ya wafanya kazi wanaostahili kuingiziwa mishahara katika Accounts zao. Kuna Taarifa ya kuwa fedha za mishahara hewa zimekuwa chakula cha Waajiri wengi Serikalini na Idara za Serikali kwani mara nyingi fedha za matumizi mengineyo (OC) huwa hazitoshi ama haziji kabisa. Hakika, suala hili la Watumishi hewa linashughulikiwa na wale ambao wamekuwa wananufaika na fedha hizo kwa hiyo wao kuwaondoa ni kama kukwamisha mipango yao na vile vile kuthibitisha ya kuwa kweli waliwaweka!Hongera sana kwa hatua hii muhimu kwa mstakabari wa Taifa letu la Tanzania.