ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 12, 2016

MIRADI YA MAENDELEO KUHIFADHIWA KWENYE KANZI DATA

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri akifuatilia utangulizi wa mapendekezo ya uundaji wa mfumo wa utunzaji wa miradi ya maendeleo – Kanzi data (Data Base), kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Omar Abdallah.

Miradi yote ya maendeleo nchini Tanzania itahifadhiwa kwenye kanzi data ili kurahisisha uratibu, upembuzi, ufadhili na utekelezaji wake.

Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

Akiongea katika ufungunzi wa mkutano wa kupata maoni ya taasisi za serikali zinazotekeleza miradi ya maendeleo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bi. Florance Mwanri alisema uwepo wa taarifa za miradi zitasadia taifa.

“Uwepo wa kanzi data hii utakuwa na manufaa sana kwa taifa kwa sababu itakuwa ni rahisi kufanya maamuzi katika mchakato mzima wa kutekeleza miradi” alisema Bi. Mwanri.

Miongoni mwa faida zitakazo tokana na mfumo huu ni kurahisisha upatikanaji wa vipaumbele vya miradi, kufanyika kwa upembuzi yakinifu vilevile upanikanaji wa fedha za kufadhili miradi hiyo. Pia mfumo huu utarahisish​​​​​​​​​​​​​​a utekelezaji na ufuatiliaji wa miradi iliyoidhinishwa na serikali
Kaimu Naibu Katibu Mtendaji – Uzalishaji, Bi. Lorah Madete, akielezea jinsi taifa litakavyonufaika na mfumo huu. Kushoto kwake ni Bi. Zena Hussein na Bw. Hekima Chengula ambao ni sehemu ya kamati ya maandalizi.
Bi. Salome Kingdom akichukua taarifa za mapendekezo ya wadau mbalimbali ya kutoka taasisi za serikali ili kuboresha uundwaji wa wa kanzi data hiyo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri akiteta jambo na wataalamu kutoka Tume ya Mipango kuhusu mrejesho wa mkutano huo.

No comments: