ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 28, 2016

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI-KUWASILISHWA KWA RIPOTI KAMILI YA UJUMBE WA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA EU

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
 
KUWASILISHWA KWA RIPOTI KAMILI YA UJUMBE
WA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA EU TANZANIA
 
ALHAMIS 2 JUNI 2016
           
 
Muangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini (Mbunge wa Bunge la Ulaya), atakuwa na mkutano na waandishi wa habari ili kuwasilisha ripoti kamili ya ujumbe huo, ikiwa ni pamoja na mapendekezo, kuhusu Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.  
 
Vyombo vyote vya habari vinaalikwa kuhudhuria:
 
Muda na tarehe: Saa tano asubuhi, Alhamis 2 Juni 2016
 
Mahali:                    Hyatt Regency Hotel, Zanzibar Room, Dar es Salaam
EU EOM ilikuwepo nchini kati ya tarehe 11 Septemba na 8 Desemba 2015, kufuatia mialiko toka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Kwa ujumla, ujumbe ulituma waangalizi 141 nchini kote kutoka nchi zote 28 wanachama wa EU, pamoja na Norway, Uswisi na Canada. Ujumbe ulitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi ulizangatia ahadi za kimataifa na za kikanda za uchaguzi, pamoja na sheria za Tanzania.

No comments: