ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 30, 2016

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA ANNETH MSUYA

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) juu ya Jeshi lake kuendelea na operesheni mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akionyesha silaha mbili aina ya bastola, zilizokamatwa katika Matukio ya Uhalifu jijini Dar leo.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikiria mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Anneth Msuya aliyeuawa kwa kuchinjwa hivi karibuni, Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa wanamshikilia mtu huyo kwa uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya mwanamke huyo.

Sirro amesema kuwa katika tukio la mauji ya mwanamke Anneth Msuya polisi wako katika upelelezi na hawezi kutaja jina la mtu wanayemshikilia kutokana na sababu za kiusalama na kuhofea kushindwa kuwakamata watu wengine.

Tukio la kuuawa kwa Anneth Msuya lilitokea Mei 26 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam, limekuwa ni mwendelezo wa matukio mengine ya uhalifu kwa familia yao yaliyowahi kutokea baada ya kifo cha kaka yake, Msuya aliyeuawa Agosti 2012 kwa kupigwa risasi, tukio lililofanyika mkoani Kilimanjaro.

Wakati huo huo majambazi wawili wameuawa kwa kupigwa na polisi na mmoja aliuawa wananchi baada ya bastola yake kuishiwa risasi huko maeneo ya Mburahati Minazini akiwa anawatupia risasi, huku mmoja akikamatwa akiwa na pikipiki aina ya boxer yenye namba za usajili MC 444 BFY na wananchi walimshambulia.

Bunduki waliokuwa nazo ni bastola yenye namba za usajili 649440  na bastola nyingine aina ya Chinese Star  ambazo silaha hizo ndizo walikuwa wanafanyia uhalifu.

Amesema pia jeshi la polisi linaendelea na operesheni mbalimbali na wanapata ushirikiano na wananchi ikiwa ni pamoja na kukamata watoto wadogo wanaotembea kundi kubwa na kuvamia na kupora kwa wananchi (maarufu panya road)

Pia alimalizia kwa kusema, Jeshi la polisi limekusanya sh. 548, 160,000 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabara kwa magari na pikipiki.

No comments: