ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 6, 2016

WANA IMANI NA MAGUFULI


masuala ya kiuchumi. Uchumi una formular zake, una principle zake. Letz abide the formulars.

Huko Amerika wakati wa Sugar Revulution "matycoon" wa huko walihujumu serikali zao hadi kuhakikisha viwanda vyote vya sukari vya serikali vimekufa ili waruhusiwe kuanzisha vyao maana vya serikali vilikua vinawawekea "kauzibe"
Sasa sitaki na sisi tufike huko. Japo tunaweza kufika huko tusipokua makini. Wale rafiki zangu wanaoimba WANA IMANI NA MAGUFULI kwenye kila afanyalo inabidi wakae kimya kidogo kipindi hiki wasije wakatuponza. Au wakizungumza wamshauri JPM kitaalamu na apime kabla ya kuchukua maamuzi.

Narudia kusema; Kumshangilia Rais na kuimba kuwa una imani nae hata anapoteleza humsaidii, unampoteza. Masuala ya kiuchumi hayatatuliwi kibabe. Lazima JPM akubali kuwa yeye ndiye aliyekosea (from the first attempt) hadi tulipofikia. Si lazima akiri hadharani kuwa alikosea. No. Anapaswa kujua Moyoni kuwa yeye ndiye kiini cha tatizo la sukari nchini.

LENGO lake lilikua JEMA lakini akatumia APPROACH isiyo SAHIHI. Akatuponza.

Kwahiyo atafute wadau wa sukari akae nao na kujadili suluhisho. Awaruhusu waingize sukari lakini ktk kiwango cha kucover deficit tu, na azuie serikali isiendelee kuigiza sukari nchini. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumesolve tatizo la sukari, wakati huo tukijipanga kutafuta long term plans ili tuzalishe sukari ya kujitosheleza na kuacha kuagiza kutoka nje.

@Malisa GJ.!

5 comments:

Anonymous said...

Hebu kalale...nchi yetu kwa sasa inabidi tuwe tumewekeza kipaumbele katika utafiti na maendeleo, uwekezaji, teknologia, na rasilimali watu...JPM yuko sawa katika hili kwani kuna wachache wanataka kutugandisha na mambo yasiokuwa na msingi...hawa jamaa wanaoficha sukali dawa yao ni jela miaka mingi tu wakanywe uji wa chumvi gelezani na siku wakitoka wachapwe viboko kumi na mbili wakawaadisie wake zao na watoto wao.

Anonymous said...

not a positive mindset, pole sana

Anonymous said...

Formula!! What works in Rome may not work in Rukwa! Formula has to be adjusted to fit applicable social economic factors and cultural and financial reality of third world countries. Copying from Developed world may or may not add anything.

Anonymous said...

Makala jipu kabisa Magufuli akae na wanaoificha sukari ilikuikomoa serikali yake kweli hii inaleta maana yeyote? Magufuli ni mtu smart na wengi wataadhirika iwe wafanyakazi au wafanya biashara kama watamchukulia Magufuli wamlinganishe na Kikwete. Inaonekana bado watanzania wengi wapo wamelala katika usingizi wa kikwete wakati kulishakucha zamani sana katika mkesha wa Magufuli.

Anonymous said...

Jamani, Kiingereza kinatupiga chenga sana. Wengine tusiojua Kiingereza yafaa tujaribu sana kuandika kwa Kiswahili; tuachanne na Kiingereza. Hata kama kuna makosa kosa ya uandishi wa lugha hii yetu, tunaweza tukaeleweka;zaidi, ni ukuzaji wa utamaduni na uzalendo wetu.

Blogu hizi zinasomwa na wengi. Tusijionyeshe kuwa nasi tumefika; kumbe, ni kujiabisha bure!