Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akisalimiana na Mwamuzi wa kirafiki kati ya timu ya soka ya Mgodi wa Buzwagi na timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama, mchezo uliopigwa kama sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Mgodi wa Buzwagi kabla ya kuanza kwa mchezo,nyuma yake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akisalimiana na wachezaji wa timu
ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama kabla ya kuanza kwa mchezo,nyuma yake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo.
Vikosi vya timu ya Mgodi wa Buzwagi na kile cha Hosptali ya wilaya ya Kahama wakisalimia kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Moja ya Hekaheka langoni mwa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakati wa mchezo wa kirafiki uliolenga kujenga mahusiano baina ya mgodi huo na wnanchi wanaozunguka eneo la mgodi huo.
Wachezaji wa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakisalimiana na viongozi mara baada ya kumalizika kwa mcheoz wa kirafiki ambapo timu ya Hospitali wilaya ya Kahama iliibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 .
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo akikabidhi kombe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kahama,Anderson Msumba aliyeongozana na nahodha wa timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama.
Wachezaji wa timu ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kombe ilipoichapa timu ya Mgodi wa Buzwagi mabao 2 kwa 1.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment