ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 2, 2016

WALIOANDAMANA UDSM WAKALIA KAA LA MOTO

Wanafunzi walioandamana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.
Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukiuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko bila kibali cha menejimenti.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga.
Alisema mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.

No comments: