ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 26, 2016

CLINTON AWAALIKA MAALIM SEIF , ZITTO

Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi
By Julius Mathias, Mwananchi jmathias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi watatu wa upinzani kutoka Tanzania na Kenya, wamealikwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Democrat nchini Marekani, unaotarajiwa kumthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu.

Walioalikwa kutoka Tanzania ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad huku kutoka Kenya akiwa ni Raila Odinga wa ODM.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis ilieleza kuwa Zitto angeondoka jana kuelekea Philadelphia, Marekani kuhudhuria mkutano huo na akiwa huko atafanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.

Pia, Ofisa Habari wa CUF, Silas Bwire alithibitisha kufahamu mwaliko huo uliotolewa kwa kiongozi huyo mwandamizi wa moja ya vyama vinayounda Ukawa. “Ni kweli amealikwa,” alisema.

2 comments:

Anonymous said...

CCM na bado,mtaisoma namba tu

Anonymous said...

Hebu fanyeni yenye maana kama kupigania katiba mpya iweze kupata ufumbuzi wa haki. Hivi mmelipiwa nauli na malazi !?