Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala ( watatu kushoto) akimsikiliza Wakaa wa Vipimo Wilayani humo, Laurent Kabikiye (aliyeshikilia mzani) wakati wa uhakiki wa mizani hiyo.
MKUU wa
Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (mwenye koti kushoto) amewaonya wanunuzi wa
Pamba Wiayani humo kuchezea mizani wanazopia zao hilo wakati wa ununuzi kwa
wakulima kwa lengo a kuwapunja wakulima na kujinufaisha zaidi. Source:Father Kidevu Blog
Kanali
Ndagala aliyasema hayo leo wakati akizindua msimu mpya wa ununuzi wa Pamba
aioufanya katika Kijiji cha Kanyonza na kusema kuwa wafanya biashara
wahakikishe kuwa mizani wanayotumia haijachezewa kwa namna yeyote na iwe
imefanyiwa ukaguzi na wakala wa vipimo.
“Leo
tunazindua ununuzi wa wa zao la Pamba katika maeneo yetu, lakini nitoe angalizo
kwa wanunuzi kuhusiana na mizani mtakayoitumia kununulia Pamba isiwe imechezewa
na kuwapunja wakulima,”alisema Kanali Ndagala.
Aidha
Kanali Ndagala aliwatahadharisha wakulima kuhakikisha pamba wanayoileta sokoni
ni Pamba safi na siyo iliyo wekwa maji au vitu vingine vyotote kama mchanga kwa
lengo la kuongeza uzito na kujipatia manufaa.
Kanali
Ndagala alisema kitendo cha kuweka maji au vitu vingine katika Pamba ni
kuharibu bidhaa hiyo na kuharibu soko kwa ujumla la zao a pambamba na
kutawafanya wanunuzi kusitisha ununuzi huo katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment