MKUFUNZI
katika Mafunzo elekezi kwa Madiwani, Lazaro Kasumbe Busiga kutoka Mradi wa
Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada
la Kimataifa la Marekani (USAID) akitoa mada ya Kanuni na Taratibu za
Uendeshaji wa Mikutano katika Serikali za Mitaa na panoja na mada ya Kanuni
kuhusu Maadili ya Madiwani kwa madiwani wa Halmashauri za Biharamulo na Kyerwa mkoani Kagera leo.
Kasumbe
ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo mkoani Dodoma,
alisema lengo la mada hiyo ni kuwawezesha madiwani hao ambao Halamashauri zao
zinaanza utekelezaji wa mradi wa PS3 Mkoani Kagera kujua taratibu muhimu
zinazotumika katika kuendesha mikutano na shughuli nyingine muhimu za serikali
za mitaa. Source: Father Kidevu Blog, Bukoba.
Mwezeshaji
wa Mradi wa PS3, kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Manumbu Daudi
akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa.
Madiwani wengi waliilalamikia taasisi hiyo kutoakana na kuchelewa kutolea maamuzi baadhi ya malalamiko ya Rushwa pamoja na kukosekana kwa ofisi za TAKUKURU katika maeneo yao na kuwataka kufungua ofisi katika ngazi ya Kata.
Mwaiswelo alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kesi nyingi za Rushwa ni kukosekana kwa ushahidi hasa pale Mtoa taarifa anaposhindwa kufika kutoa ushahidi.
Pia
alisema lengo linguine ni kumpa Diwani ufahamu muhimu juu ya kanuni za Maadili
ya Madiwani ili kumwezesha kuwa na mwenendo unaotazamiwa na jamii anayoitumikia
katika maisha ya utekelezaji wa majukumu yake.
Mafunzo
hayo yanamuwezesha Diwani kuainisha mahitaji muhimu ya uendeshaji wa vikao,
kueleza maana na dhana ya akidi ya mikutano na vikao, kuainisha mambo muhimu
wakati wa maandalizi ya mikutano pamoja na kumuwezesha diwani kuanisha taratibu
za uundaji wa Kamati za kudumu.
Aidha kwa
upande wa mafunzo juu ya Kanuni kuhusu maadili ya Madiwani yatamuwezesha diwani
kuainisha kanuni za maadili ya madiwani , kuzingatia maadili hayo wakati wa
utekelezaji wa majukumu yake na yatamfanya diwani kutambua mahusiano ya
kiutendaji kati yake na watumishi wa halmashauri.
Washiriki wakiuliza maswali mbalimbali kutokana na mada zilizo wasilishwa na wawezeshaji.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Wakuu wa Wilaya za Kyerwa, Kanali (Mstaafu) Shaaban Lissu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Wende Ng'ahala wakifuatilia mada hizo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Maofisa wa PS3 wakiwajibika kuhakikisha mambo yanaenda vyema (picha ya juu) huku Wataalam wa Masuala ya Utawala wa Mradi wa PS3 wakifuatiia mijadala kwa umakini na kuitolea ufafanuzi.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde akichangia hoja mbalimbali.
No comments:
Post a Comment