
Dkt Leonard Maboko
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama
Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Taarifa ya Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07
Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi
huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt. Leonard
Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye
mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es salaam
08 Julai, 2016.
No comments:
Post a Comment