Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesitisha maandamano ya UKUTA ambayo yalipangwa kufanyika Septemba 1 (kesho) baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini.
Akiongea na waandishi wa habari muda huu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema chama kimeona kisitishe maandamano kwa muda ili kiwaachie viongozi wa dini watafute suluhu kuhusu suala hilo.
“CHADEMA tunaomba kuwatangazia watu wote kwamba tunahairisha mikutano ya kisiasa na maandamano yote kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Freeman Mbowe
5 comments:
Hapakuwa na chochote hapo. Nani mjinga angeacha kazi zake kufuata ujinga wa wanasiasa wanaojitafutia umaarufu. Magufuli alishinda muacheni afanye yake mkutane uchaguzi ujao. Msiwapotezee watu muda wao.
What breaking news? One must have been too dumb not to see this coming. These guys are just playing games. They keep loosing their credibility each passing day.
Hawa jamaa wa Moshi/Arusha wasirubuni wananchi. They have the time and money to waste.
Unadaiwa rent unaitisha maandamano nchi nzima!
hii ndio kula ya watu wengine. kisha wemgine wanafuata mkumbo. kalipe pango kwanza
Post a Comment