ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 10, 2016

Lissu ahofia kuvuliwa ubunge (Video)

By Fidelis Butahe, Mwananchi fbutahe@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amezihusisha barua walizoandikiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na njama za kutengeneza mazingira ya kuwakosesha viongozi wa chama hicho sifa za kuwa wabunge.

Lissu, ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki, na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na mbunge wa Hai, wameandikiwa barua na sekretarieti hiyo wakitakiwa wajieleze kuhusu kauli zao za hivi karibuni.

Lakini Lissu, ambaye jana aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa na katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, alisema barua hiyo imeandikwa kienyeji na kutozingatia taaluma ya sheria kutokana na kutoeleza tuhuma zao na kauli wanazotuhumiwa kuzitoa.

Pamoja na kutotaja tuhuma hizo, viongozi hao wa Chadema waliingia kwenye mgogoro na Jeshi la Polisi na baadaye Mbowe na Lissu kuitwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kuhojiwa. Baadaye Lissu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kwa uchochezi.

No comments: