UONGOZI wa Shule za Feza nchini umeibuka
na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa wao
hawana uhusiano na Fethullah
Gulen wala serikali ya Uturuki kwa
vile hawajawahi kupokea misaada toka
pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.
Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule
za Feza zipo hatarini kufungwa kwa madai
kuwa mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama
asasi zingine zilizosajiliwa kishera na
serikali, hivyo ni mali ya watanzania.
“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda
cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania
na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.
Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za
awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.
Aliongeza kuwa huo ni
uwekezaji wenye mchango katika kukuza
pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais
John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake
zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.
Alisema
wanatoa wito kwa wazazi kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa
manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment