Kaimu katibu mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umetangaza kusitisha maandamano waliyokuwa wamepanga kuyafanya Jumatano hii ili kuunga mkono juhudi na kazi inayofanywa na Rais Dk John Magufuli.
Umesema kuwa umepokea majibu ya barua yao kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu inayowataka kuacha kufanya maandamano yao kwa sababu polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na maandamano nchi nzima.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka, ilisema mbali na barua hiyo pia wamefikia uamuzi huo unatokana na utii, nidhamu na kuzingatia utaratibu wa mamlaka za juu ndani ya chama.
CHANZO: HABARI LEO
No comments:
Post a Comment