Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nje wa nchi za Jumuiya ya Madola.
Waziri Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah
Waziri katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti, Bw Sabah Al KHalid Ala Sabah
Waziri Mahiga alipoongoza kikao cha Troika ya SADC
Waziri Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah
Waziri alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Belgium Bw. Alexander De Croo
Na Mwandishi Maalum, New York
Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali, kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa takribani wiki nzima iliyopita wameendelea kuelezea vipaumbele vya nchi zao mbele ya wajumbe wanaohudhuria Baraza Kuu la 71 la UMoja wa Mataifa.
Mambo makubwa ambayo karibu kila kiongozi ameyagusia katika hotuba yake ni pamoja na tatizo la kuongezeka kwa matukio ya ugaidi, tatizo la wakimbizi na wahamiaji, vita na machafuko vinavyoendelea katika nchi kadhaa, ubaguzi kwa misingi ya dini au eneo analotoka mtu, mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Pamoja na viongozi hao kushiriki katika majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu, lakini pia wamekuwa wakishiriki mikutano mingine ya pembezeni ambayo imeandaliwa sambamba na mkutano mkuu.
Aidha mikutano ya kimataifa na mikubwa kama huu wa 71 wa Baraza Kuu pia hutumika na viongozi wakuu na wa nchi na serikali kama sehemu ya kukutana na kufanya mazungumzo na kuweka mikakati ya mahusiano baina ya nchi zao.
Kama ilivyokuwa kwa Viongozi wengine, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Dkt.Augustine Mahiga ( Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia ametumia fursa ya mkutano huu kukutana na viongozi wengine na kubadiliana mawazo na kujadiliana miongoni mwao mambo kadha wa kadhaa yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo Mhe. Waziri Mahiga ameshiriki nje ya majadiliano ya Jumla. Leo Jumatatu Waziri atapata fursa ya kuelezea vipa umbele vya Tanzania wakati atakaposoma hotuba yake.
No comments:
Post a Comment