Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwinga akihutubua wananchi wakati Tigo walipotoa madawati mia moja kanda ya ziwa.
MKUU wa wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa amefanya operesheni maalumu ya siku mbili katika Misitu ya Hifadhi ya North Ugala na kuteketeza nyumba za kaya120 zilizojengwa kinyemela katika hifadhi hiyo ya
wanyama pori.
Operesheni hiyo imeenda sambamba na uteketezaji makazi ya wavamizi hao kwa kuchomwa moto huku mengine yakibomolewa ili kudhiti vitendo vya uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa katika hifadhi hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo DC Kwingwa alisema operesheni hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Tebela kata ya Iyumbu Wilayani humo na maeneo yote yanaozunguka hifadhi hiyo itakuwa endelevu ili kuimlisha
uhai wa mistu ya hifadhi wilayani hapo.
Aidha alisema Operesheni hiyo imefanikuwa kutokana na ushirikiano mzuri walipata kutoka kwa viongozi wa Serikali ya kijiji na kata kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Ili kudhibiti wavamizi hao aliagiza askari wa doria na vikosi vyote vinavyohusika kulinda Hifadhi hiyo kufanya msako kila baada ya wiki mbili ili kubaini wavamizi watakaojaribu kurudi katika kihifadhi hiyo
ili wakamatwe.
‘Zoezi hilo litakuwa endelevu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu ama kikundi chochote cha watu kitakachobainika kurudi kufanya shughuli zake katika hifadhi hiyo’, alioongeza. Alitaja uharibifu uliofanyika katika hifadhi hiyo kuwa ni ukataji miti ovyo uliosababisha kuondoka kwa wanyama pori, uchomaji wa mkaa pasipo
kufuata sheria, uvunaji wa mbao na magogo, ujenzi wa nyumba za makazi kinyume na taratibu za sheria za hifadhi.
Alibainisha kuwa serikali haiko tayari kuona maeneo ya hifadhi yakiendelea kuharibiwa na watu wachache wasio na nia njema huku akionya kuwa sheria itachukua mkondo wake ili kudhibiti hali hiyo na
hawatasita kuharibu makazi yanayojengwa katika maeneo yalitengwa kwa ajili ya hifadhi.
Katika opesheni hiyo DC aliongozana na kikosi cha askari wa doria,viongozi wa WMA, Afisa Uhamiaji na Maofisa wa Magereza Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Florence Mwala.
No comments:
Post a Comment