Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje(Picha kutoka Maktaba)
Na: Frank Shija, MAELEZO
Ukubwa wa deni la taifa siyo jambo linaloweza kusababisha kuyumba kwa uchumi wa nchi, kinachooneka ni kuendela kuaminiwa kwa Tanzania ndani na nje ya nchi jambo linalopelekea tuna pata fursa ya kukopesheka kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Profesa Haji Semboja alipofanya mahojiano maalum na mwandishi kutoka Idara ya Habari, MAELEZO kuhusu hali ya uchumi ilivyo kutokana na ongezeko la deni la Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
“Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya, ni mzigo wa kimaendeleo. Unnecessary devil” Alisema Profesa Semboja.
Aliongeza kuwa kutokana kwa imani waliyo nayo wahisani ndani na nje ya nchi ndiyo maana washirika wetu wanatukopesha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama ambavyo tumeshuhudia ujenzi wa Daraja la Kigamboni, hivi karibuni tutanufaika na usafiri wa ndege”. Alisema Profesa Semboja.
Aidha amempongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli kwa hatua alizochukua za kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuondoa safari za nje zisizo za rasmi pamoja na kupiga vita vitendo vya rushwa.
Semboja aliendelea kusema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni Serikali ya awamu ya Tano kulipa madeni ya watangulizi wake huku ikitekeleza miradi ya maendeleo jambo linaloongeza imani miongoni mwa wahisani.
Hata hivyo alionya juu ya matumizi mabaya ya rasilimali fedha kuwa zinasababisha kushindwa kutekeleza wajibu wa kulipa deni kwa wakati na kupelekea kulimbikiza madeni jambo ambalo si sahihi.
Alitajaa baadhi ya matumizi mabaya ya fedha kuwa ni pamoja na safari za nje na ndani ya nchi zisizokuwa na tija, ulevi, kupelekea fedha katika miradi isiyopangwa na mengine.
Wananchi wametakiwa kutoyumbishwa na waelewi kuwa kupitia fedha zinazokopwa wanufaika wakuu ni wananchi wenyewe, mfano fedha zitakazo tumika kujenga Nyumba za Magomeni ambazo Mhe. Rais amehaidi waliokuwa wakazi wake kuishi bila kulipia kwa kipindi cha miaka mitano zikitokana na mikopo hiyo wananufaika.
1 comment:
Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya?? Huyu ndiyo aina wa maprofesa waliosoma kwenye nchi za kijamaa ambazo propaganda ndiyo maisha ya kila siku. Hivi kweli ukubwa wa deni la taifa ambalo limetumika kwa kununulia maandazi ya chai cha maofisini, safari za nje na mengineyo siyo mzigo mbaya?? Amesema tunafaidi ndege....Je wananchi wa kawaida wanafaidikaje na hizo ndege mbili? Je ndege siyo usafiri wa kawaida ambao wananchi kama wana uwezo wanalipia kwa pesa zao? Kabla hata hizo ndege za ATC za propaganda mbona zilikuwepo za Precision na Fast jet ingawa usafiri wa ndege haujawa mkubwa nchini? Profesa wananchi hatufaidi usafiri wa ndege, kwa wenye uwezo wanaulipia kwa pesa za jasho lao na wenye ndege wanafanya biashara kama biashara zingine, Acha porojo za kisiasa!!!!
Post a Comment