Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2016
amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Songwe.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.
Bw. Eliya Mtinangi
Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana tarehe 09 Septemba, 2016
ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa
wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi
wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1
na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi
katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi
walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1.
Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa
ya Dodoma
2.
Elias R. Ntiruhungwa - Mji wa Tarime
3.
Mwantumu Dau - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
4.
Frank Bahati - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
5.
Hudson Stanley Kamoga - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
6.
Mwailwa Smith Pangani - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
7.
Godfrey Sanga - Halmashauri ya Wilaya
ya Mkalama
8.
Yusuf Daudi Semuguruka - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
9.
Bakari Kasinyo Mohamed - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
10. Juma Ally Mnwele - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
11. Butamo Nuru Ndalahwa - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
12. Waziri Mourice -
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
13. Fatma Omar Latu - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
Wakurugenzi wa
halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne tarehe 13
Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
No comments:
Post a Comment