Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
|
27 Oktoba, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Majibu ya Ubalozi wa Marekani kwa Tamko la Wizara ya Afya la Oktoba 25
Dar es Salaam, TANZANIA. Marekani inathamini kwa kiasi kikubwa ushirikiano
wake wa muda mrefu na wenye mafanikio na nchi ya Tanzania katika sekta ya afya,
hususan maendeleo ambayo Tanzania imeyapata katika mwitikio wake duniani kuhusu
maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi chini ya ufadhili wa Mpango wa
Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR). Tumedhamiria kufanya
kazi na Tanzania katika kukabiliana na janga la VVU/UKIMWI kwa ujumla na kwa
hivyo basi, tumelipokea tamko la Oktoba 25 la Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu,
ambalo limesisitiza dhamira ya serikali ya Tanzania kutoa huduma ya afya na VVU
kwa raia wa Tanzania wote bila ubaguzi. Pia, tunaishukuru serikali ya
Tanzania kwa kukubali viwango vya shirika la afya duniani (WHO) na taratibu
zinazokubalika kimataifa katika kinga na tiba, pamoja na mwongozo wa kutoa huduma
kwa Makundi Maalum. Dhamira ya wazi ya waziri kufanya kazi na
washirika, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoisaidia
serikali ya Tanzania katika eneo hili itasaidia kuhakikisha huduma zinawafikia
watu na sehemu zinakohitajika zaidi, ikiwa ni pamoja na takriban wanaume,
wanawake na watoto milioni 1.4 wanaoishi na VVU/UKIMWI nchini kote. Serikali ya
Marekani inaunga mkono mwendelezo wa ushirikiano huu na Tanzania katika
kukabiliana na majukumu ya kiafya nchini, pamoja na lengo letu la pamoja la
Kizazi Huru dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.
Kwa taarifa zaidi kuhusu
hafla hii, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga
(SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani, Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment