Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.
Shule ya sekondari ya Almuntazir iliyopo upanga jijini Dae es
salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi
wa mazingira kwa kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani ya eneo
la mikoko katika eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila
kuzingatia mita sitini zinazotakiwa kisheria.
Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na
ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina iliyofuatia malalamiko ya wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri
kufanya ziara yakwenda kujionea uchafuzi huo.
Akiongea kwa Niaba ya shule meneja wa shule hiyo Bw. Serialis
Rwechungura amesema kuwa, watalipa faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali
na hakuwa tayari kuongelea swala la ukuta wa shule hiyo.
Naibu Waziri Mpina amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari
kuwavumila wawekeajia wakiukaji wa sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani
maisha ya watanzania.
Aidha Naibu Waziri alitembelea maeneo ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa
mazingira uliotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu
ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo
ya mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa ya
maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.
Akiikemea DAWASCO kwa mara nyingine kwa kutokuonyesha
uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu, Naibu Waziri Mpina ameita NEMC
kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kutelekeza
miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.
No comments:
Post a Comment