Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo kwa vyombo vya habari kuhusu Mkutano wa Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia unyonyaji na usafirishaji wa watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono unaoendelea leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga pamoja na baadhi ya Wajumbe wa bodi ya Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono Duniani wakifuatilia maendeleo ya Mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono leo jijini Dar es Salaam.
NA ANTHONY ISHENGOMA
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Sihaba Nkinga leo amefungua mkutano
wa mashauriano wa kanda ya Afrika kuhusu Mtandao wa Kuzia Unyonyaji na Usafirishaji wa Watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono.
Akiongea katika
Mkutano huo Bi Sihaba Nkinga amesema Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika imeridhia na kutekeleza mikataba mbalimbali ikiwemo
kutunga sera na sheria pamoja na
mikakati ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto.
Aliendelea kusema mwaka huu Tanzania ni Nchi pekee barani
Afrika ambayo imechaguliwa kama nchi ya kuigwa kwenye juhudi za dunia kupambana
ukatili wa wanawake na watoto akizataja Nchi nyingine kuwa za Mexico, Indonesia
na Sweden.
Katibu Mkuu Sihaba Nkinga amesema kuwa Tanzania imechaguliwa
kuwa moja ya Nchi zinazounda ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ukatili
wa Wanawake na Watoto kwasababu ilikuwa Nchi ya pili duniani kuitikia wito wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa
kufanya tafiti za ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto barani Afrika.
Akiongea katika Mkutano huo wa mtandao wa kuzuia unyonyaji
kingono kwa watoto Afrika Bi. Sihaba Nkinga amesema taarifa ya utafiti huo ilyofanyika mwaka 2009
na kusambazwa mwaka 2011 ilitoa majibu ya yaliyonesha kuwepo kwa ukatili dhidi
ya wanawake na watoto katika ngazi zote ikiwemo ngazi ya familia, shule na
njiani kuelekea shuleni.
Aidha ameviambia vyombo vya Habari vilivyokuwepo katika
Mkutano huo kuwa hii ndio sababu kwasasa Tanzania inajipanga kuzindua Mpango
Mkakati wa kupambana na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema
tarehe 13 mwezi desemba.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la KIWOEDE Bi.
Justa Mwaitaka amesema mtandao huu unakutana kujadili namna bora ya kupeana
taarifa za Watoto wanaosafirishwa kwa lengo la kunyonywa kingono ndio maana
kuna Nchi 21 kutoka barani Afrika.
Aliongeza kuwa Mkutano huu utaangalia sheria zilizopo kama
zinakidhi haja ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto akizitaja sheria za
Tanzania kuwa na utaratibu unaochelewesha upatikanaji wa haki za watoto pindi
inagundulika kuwepo kwa ukatili dhidi ya watoto taratibu za kisheria na
kimahakama zinakuwa ngumu katika utekelezajia wake.
No comments:
Post a Comment