ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 29, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO AZINDUA HUDUMA MPYA YA KIKUNDI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dorothy S. Mwanyika (wa pili kutoka kushoto)Akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Accessbank Bi Hedvig Sundberg(wa pili kutoka kulia ) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara, Ndugu Andrea Ottina (kulia)Mwakilishi kutoka shirika la Care International Ndugu Christian Pennotti (kushoto) Akizungumza kwenye uzinduzi wa Huduma Mpya Ijulikanayo Kama KIKUNDI Inayotolewa na Access bank Mhe. Dorothy S. Mwanyika amewataka watanzania Kujiunga Kwenye Vikundi Mbalimbali na kisha Kuchangamkia Fursa hiyo inayowawezesha wana kikundi Kujipatia Huduma Mbalimbali za Kibenki Kupitia Simu ya Mkononi Kwa Haraka na yenye usalama zaidi.

Huduma Hii inawapa uwezo wanakikundi kuweza kufanya Mihamala ya Benki muda wowote na Mahali popote walipo kwa kutumia Simu. 
Uzinduzi huo pia umeudhuriwa na Mdau Mkubwa wa Maendeleo Mwakilishi kutoka shirika la Care International Ndugu Christian Pennotti (kulia)Ambapo amesema Kwa sasa Hapa Tanzania shirika hilo linasimamia vikundi zaidi ya 10,000 vyenye wanachama zaidi ya 250,000 vikundi hivyo vimekua na uhitaji mkubwa wa huduma za kisasa za kibenki jambo ambalo Wameishukuru AccessBank kwani wamekua mojawapo ya Mabenki wanaounga mkono na kuhakikisha vikundi hivi vinapatiwa huduma za kibenki tena kwa njia za kisasa kabisa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dorothy S. Mwanyika Akizindua rsmi Huduma ya KIKUNDI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dorothy S. Mwanyika Akikata keki wakati wa uzinduzi huo.
Akizungumza pia juu ya hili, Afisa Masoko wa AccessBank Ndugu Sijaona Simon alisema "Kwa bahati mbaya, kwa muda mrefu vikundi vya aina hii vimekuwa vikitengwa na taasisi mbali mbali za kifedha ikiwa ni pamoja na mabenki hii ni kutokana na huduma kuwa ghali mnohuku zikiamabatana na masharti magumu ya nyaraka zinazohitajika. Akaunti hii ya KIKUNDI ni mahususi kwa ajili yao"Mpaka sasa vikundi zaidi ya 100 vimeshajiunga na AccessBank Tanzania na tunatarajia vikundi vingi kujiunga na akaunti hii.”

Kwa kawaida vikundi hivi huwa na jumla ya wanachama 15 hadi 30, wanachama hawa hukukutana kwa wiki mara moja kwa lengo la kununua hisa, kukopeshana na kujadili masuala mengine ya kijamii ikiwa ni pamoja na ustawi wa jamii inayowazunguka. Fedha zote huhifadhiwa ndani ya kibubu, na wanachama watatu hukabidhiwa funguo za kibubu hicho.Kwa kawaida kikundi huwa na Viongozi watano ambao huchaguliwa na wanachama, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti, Wahasibu wawili, Katibu na Mweka Hazina.Wanachama wengine watatu ambao hushikilia funguo za kibubu ambacho hufunguliwa mara moja kila wiki baada ya mkutano kuanza. Licha ya usalama wa mfumo wa funguo, njia ya kuhifadhi fedha kwenye kibubu imeonekana kuwa si chaguo salama kwani mara nyingi huweza kuibiwa hasa mwishoni mwa mzunguko ambapo fedha zilizohifadhiwa kwenye kibubu huwa zimefikia kiasi kikubwa. Kutokana na haya , Access Bank imeamua kuja na njia mbadala ya kibubu kwa kuanzisha akaunti iyakayounganishwa na simu ya mkononi ambapo sasa kila muamala utakaofanyika utaanzishwa na Mwenyekiti na kupewa idhini na Waweka hazina wawili kupitia simu zao za mkononi. 

AccessBank WAKALA , ni mawakala wanaotoa huduma za kibenki kwa niaba ya AccessBank watapatikana maeneo ya karibu na vikundi ili kuweza kurahisisha huduma ya kuweka na kutoa fedha kwa haraka zaidi. Tofauti na kuweka fedha kwenye akaunti ya kikundi ambapo idhini ya watu wengine haihitajiki ,kutoa fedha kwenye Akaunti kutahitaji idhini kutoka kwa wanachama watatu.Vikundi hivi kwa kupitia Akaunti ya KIKUNDI inayowezeshwa na AccessMobile vitaweza kunufaika na huduma za AccessBank kwa kufanya miamala ya bure kwa njia ya simu ya mkononi na kuungana na watumiaji wengine wa huduma hii.

No comments: