Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mapema hii jana mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akikakagua uchafuzi wa mazingira unaofanywa na gereza la keko lililopo temeke jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Luhaga Mpina akifanya akipita pembezoni mwa mfereji wa maji
taka, ambapo uko karibu na makazi ya watu
Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina (Mb.) Amelitoza faini ya shilingi milioni thelathini Gereza la keko kwa kosa la kutiririsha maji
taka yanayozalishwa gerezani hapo hivyo
kuhatarisha maisha ya Binadamu na viumbe hai wengine.
Akiwa katika ziara nyingine ya ukaguzi wa mazingira jijini
Dar es Salaam, Naibu Waziri Mpina Alilitaka Baraza hilo kutoa agizo kwa mkuu wa
gereza hilo litakalokuwa na maelekezo ya
kujenga miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira sambamba
na kulipa faini hiyo kwa muda uliyotajwa.
“Taasisi za Serikali zinapaswa kuwa mfano kwa kutii sheria za
nchi hususani sheria ya mazingira nimeshasema mara nyingi na ninarudia hapa
tena taasisi za serikali haziruhusiwi kuchafua mazingira kwa namna yoyote ile
kwa mujibu wa sheria. “ alisisitiza Mpina.
Aidha Mpina ameitaka Manispaa ya Temeke kusimamia kuwa makini
na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya Keko na kuwachukulia hatua
wananchi wote wanaotiririsha maji taka katika mifereji ya maji ya mvua.
Akitoa ufafanuzi wa adhabu hiyo mwanasheria wa Baraza la
mazingira, Suguta Heche, amesema kuwa Tasisi
za serikali na mashirika ya umma yana wajibu wa kufuata sheria za nchi hususani
sheria za mazingira na ukiukwaji wa sheria hizo utaambatana na adhabu kama
zinatolewa kwa mashirika na makampuni binafsi.
Awali Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kutengeneza
dawa cha Keko Pharmaceutical limited
na kutoridhishwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho wa
kutiririsha maji taka katika makazi bila kutibiwa, na kutokuwa na kibali cha
utiririshaji kutoka kwa bonde na kuwatoza faini ya shilingi milioni ishirini
inayopaswa kulipwa ndani ya wiki mbili, na kuelekeza usafi wa mazingira
kufanyika katika mifereji ya maji ya mvua na kuwaasa wakazi wa maeneo jirani
kutokutupa takataka katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Bwana Selemani Ndugwana, Meneja uthibiti na Ubora
wa kiwanda hicho cha dawa alipokea adhabu hiyo, na kusema kwamba ni kubwa sana
wanaomba serikali iwapunguzie adhabu hiyo, kwa kuwa ni kosa la mara ya kwanza.
Akiwakilisha wakazi wa eneo la keko mtendaji wa kata hiyo Bwana Samweli Magali
alisema kero ya uchafuzi wa mazingira unaotoka kwenye kiwanda hicho cha madawa
ni kubwa na ni hatarishi kwa afya za wakazi wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment