Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipofanya ziara ya kukagua zoezi la uhawilishaji wa fedha katika Wilaya ya Kishapu. Katika zozei hilo alijionea namna ambavyo walengwa kutoka kaya maskini wanavyopata ruzuku.
Aliwataka walengwa kutumia fedha wanazopata kwa usahihi na kujikita katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi. Mkuu huyo wa mkoa katika ziara hiyo alizuru vijiji vya Mipa, Seke Ididi na Dulisi kata ya Seke Bugoro
Katika ziara hiyo aliambatana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Josephine Matiro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Boniphace Butondo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Mratibu wa TASAF Wilaya, Rehema Edson na viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza na wananchi wanufaika wa Mpango wa TASAF katika ziara hiyo.
Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kishapu, Rehema Edson akitioa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa na viongozi mbalimbali kuhusu zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa alipofanya ziara wilayani humo.
Mmoja wa walengwa wa TASAF akichangia jambo wakati wa ziara hiyo.
Sehemu ya wananchi walengwa wa Mpango wa TASAF wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua zoezi la TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akifurahia jambo na wananchi wanufaika wa Mpango wa TASAF wilayani Kishapu.
Walengwa wa TASAF wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack.
No comments:
Post a Comment