Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa TanzaniaDkt. John Pombe Joseph Magufuli (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakisaini makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakionyesha mikataba ya makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia iliyotiwa saini leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe. Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (nyuma mwenye tai nyekundu) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania Balozi John Kijazi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu (hayupo pichani) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mgeni wake Rais wa
Zambia Edgar Lungu (mwenye tai nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi kutoka Tanzania na Zambia leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank
Shija – MAELEZO.
Na. Immaculate
Makilika – MAELEZO
SERIKALI za Tanzania
na Zambia zimeahidi kuimarisha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na mradi
wa bomba la mafuta la TAZAMA yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa baina ya nchi hizo.
Akizungumza leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Zambia
Mheshimiwa Edgar Lungu alisema kuwa Tanzania
na Zambia zitaendelea kushirikiana
kuiboresha reli hiyo ili iweze kufanya kazi
kwa ufanisi.
Kwa upande Rais John
Pombe Magufuli alisema reli ya TAZARA na
bomba la mafuta la TAZAMA zinakabiliwa na changamoto za mtaji na uongozi na
hivyo kufanya reli hiyo kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 128,000 tu,
ambapo ilipoanzishwa mwaka 1976 ilikua na uwezo wa kubeba mizigo tani 500,000.
Ili kutatua
changamoto hizo Rais Magufuli alisema kuwa “tumekubaliana kubadilisha menejimenti ya TAZARA, kubadilisha sheria ili
kuwezesha menejimenti hiyo kuongozwa na
mtu mwenye uwezo ambaye si lazima
awe anatoka Tanzania au Zambia”.
“Nia ya Serikali hizi
ni kuongoza reli hiyo kibiashara kwa
maslahi na maendeleo ya nchi zote mbili” alisema Rais Magufuli.
Kwa mujibu wa Rais
Magufuli malengo ya Serikali zote mbili ni kupunguza ucheleweshaji mizigo kufika nchini Zambia, ambapo wamekusudia kupunguza vituo vya kukagua magari ya mizigo
hadi kufikia vinne.
Rais Magufuli alisema
mbali kujenga kituo kimoja cha forodha huko Tunduma, ambapo kwa upande wa
Zambia tayari wameshajenga kituo hicho na kwa upande wa Tanzania wanatarajia
kujenga kituo chake baada ya mwaka mmoja na nusu kutoka sasa.
Sambamba na hayo Serikali hizi mbili zimesaini
makubaliano ya kuwepo kwa mashaurinao ya kidiplomasia, pamoja na kuahidi
kuendeleza ushirikiao wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.
No comments:
Post a Comment