Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kulia) alipotembelewa na balozi huyo leo Jijini Dar es Salaam ambapo walizungumza kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimueleza jambo Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) alipotembelewa na balozi huyo leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Denmark nchini Bibi.
Camilla Christensen (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wakijadiliana kuhusu Sheria ya
Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa
Denmark Nchini Bw. Einar Jensen. Picha
na Lorietha Laurence
Na
Lorietha Laurence-WHSM
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Sheria
ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ipo kwa ajili ya manufaa ya kuendeleza sekta
ya habari, wanataaluma na Taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Jensen ambapo aliuliza kuhusu
malalamiko ya waandishi wa habari kupoteza ajira kufuatiwa kuwepo kwa sheria
hiyo.
Mhe. Nape alifafanua kuwa sheria hiyo imetoa
kipindi cha muda wa miaka mitano kwa wanahabari wasiokuwa na shahada ya kwanza
kuweza kujiendeleza kimasomo ili kukidhi sifa za mwandishi wa habari.
“Sheria
hii tayari imeshasainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli ambapo kwa sasa tupo
katika utaratibu wa kuweka kanuni mbalimbali ili kufidia sehemu zenye mapungufu”
alisema Mhe. Nape
Anaongeza
kwa kueleza kuwa kuna faida mbalimbali zinazomsaidia mwandishi kunufaika na
sheria hii ikiwemo bima ya Afya na mfuko
wa mafunzo kwa wanahabari ambapo watawezeshwa kupata mkopo wa kujiendeleza
kielimu.
Naye
Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo
nzuri na kuomba ofisi ya Ubalozi wa Denmarm kupatiwa nafasi ya kuweza kukutana
na Waziri kwa ajili ya kupata elimu kwa kina kuhusu sheria hiyo.
Sheria
ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ilipitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mkutano wake
wa 5 mjini Dodoma na kusainiwa na Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Novemba mwaka juu.
No comments:
Post a Comment