hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali
la Ilula Ophan program (IOP)
na Fredy Mgunda,Iringa
Shirika lisilo la kiserikali
la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za
utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.
Akizungumza na blog hii Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) Edson Msigwa alisema
kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la wamasai bado ni kubwa.
Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya
shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya
wamasai
“Tunajitahidi kuwafikia
jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu lakini
tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu hasa
huku umasaini”alisema Msigwa
Aidha Msigwa alisema kuwa
kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini na kuitaka serikali kukubali takwimu
wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.
“Sisi hapa Ilula Ophan
program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai wafanikiwa kukimbia
kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa
aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa
kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa
Naye mmoja wa wasichana wa
kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce Hassani alisema kuwa msichana
wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.
“Mimi na mwenzangu tumemaliza
shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka kutuozesha lakini mungu mwema
tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa
wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi
kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce
Joyce ameiomba serikali na
mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila potofu
zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.
“Angalia tunavyoteseka saizi
tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana afya zuri kabisa
lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa tukiwa na umri
mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema
Joyce
Zipo sababu nyingi na
ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo
ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.
Wasichana wanaopata ujauzito
na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula -
Vescovaginal fistula.
Kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA) umeonesha kuwa
katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni
yaliripotiwa nchini tanzania.
No comments:
Post a Comment