ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 14, 2016

NEC YAENDELEA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI MJINI ZANZIBAR.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva  akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani mjini Zanzibar leo  Desemba 14, 2016 . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan.
  Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Mstaafu Mary Longway akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Desemba 14, 2016 mjini Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid  (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao  cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume mjini Zanzibar leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kulia).
 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Prof. Amon Chaliga akieleza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar. Kulia  ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid (katikati).
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumza na Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Zanzibar kwenye kikao cha maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar leoDesemba 14, 2016. Picha na Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

No comments: