Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Elias Mwita aliwaeleza waandishi wa habari kuwa saa tatu asubuhi jana mwanamke huyo alikamatwa na majirani zake chumbani kwake alikopanga eneo la Kitangiri na kisha kutoa taarifa polisi.
Mwita alisema mwanamke huyo alikamatwa na Polisi kwa tuhuma ya kumtupa mtoto wa siku moja chooni baada ya kujifungua Ijumaa wiki iliyopita, na kwa mujibu wa maelezo yake baada ya kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho.
“Baada ya tukio hilo na mtu kutojulikana aliyefanya kitendo hicho, tulitoa wito kwa wananchi ili kuweza kumbaini, lakini juhudi za wananchi za kumsaka zimezaa matunda sasa majirani wameweza kumbaini mwanamke huyo ndiye aliyehusika na unyama huo, lakini amekiri kuhusika na utupaji wa mtoto,” alieleza Kamanda Mwita.
Hata hivyo, Mwita alisema saa tisa ya Januari 21, mwaka huu mwanamke huyo alionekana kwenye eneo la kanisa hilo, na baada ya kumhoji kwa mujibu wa maelezo yake, alieleza kuwa alikwenda chooni kwa lengo la kujisaidia, lakini ikatokea bahati mbaya mtoto kutumbukia kwenye tundu la choo.
Aidha, Kamanda Mwita alisema kinachofuata ni utaratibu wa sheria wa kumfikisha mahakamani ili kujibu tuhuma hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Habiba Jumanne aliwaeleza waandishi wa habari kuwa saa 11 ya Januari, mwaka huu alipigiwa simu na baadhi ya waumini wa kanisa hilo kuwa kuna mtoto mchanga wanasikia sauti yake ndani ya tundu la choo.
Jumanne alisema mtoto huyo mwenye siku moja alikutwa kweli kwenye tundu la choo akiwa hai baada ya waumini wa kanisa hilo na askari kubomoa choo na kumtoa mtoto huyo kisha kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, ambako hata hivyo alifariki dunia.
Hata hivyo, alitoa mwito kwa jamii kuacha mara moja vitendo vya kinyama na kama wanaona maisha magumu kulea watoto wawapeleke kwenye mashirika au taasisi za kulea watoto wakapate kukua kuliko kutenda unyama wa mauaji, pia washirikiane kubaini aliyefanya kitendo hicho atakuwa sio mtu wa mbali katika makazi ya eneo hilo.
Mzee wa Kanisa hilo, David Madata alisema ni bora mwanamke huyo baada ya kujifungua angempeleka kwenye taasisi mbalimbali kama alishindwa kumlea kuliko unyama alioufanya.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment