ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 10, 2017

ASKOFU MOKIWA: MIGOGORO ANGLICANA NI YA KUPANDIKIZWA

Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, amesema migogoro mingi inayotokea katika kanisa hilo ni ya kutengenezwa jambo linalowavunja mioyo waumini.
“Kanisa ndilo kimbilio la waumini wenye shida mbalimbali, sasa kukiwa na migogoro waumini watamkimbilia nani?” alisema
Dk Mokiwa alizungumza hayo jana na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini, Jacob Chimeledya alimtaka Dk Mokiwa ajiuzulu.
Askofu Chimeledya alimtaka Askofu Mokiwa ajiuzulu kwa kile alichodai kuwa anatumia madaraka yake vibaya na ubadhirifu wa fedha.
Hata hivyo, katika kikao chake na wanahabari leo asubuhi, Askofu Mokiwa alikanusha na kudai kuwa migogoro hiyo inapandikizwa na maadui zake.

No comments: