Wednesday, January 25, 2017

Kwa nini uchoshwe na chakula cha usiku?

Uhali gani shoga yangu? Kiafya mwenzako kama ulivyoniacha jana, kama ni mzima ni jambo la kumshukuru lakini pia kwa wale wagonjwa nawaombea Mwenyezi Mungu ataweka wepesi! Baada ya hayo, nigependa kuzungumza na wewe shoga yangu kuhusu athari za kumwambia mumeo umechoka.
Najua unatoa macho na kushangaa! Shoga, kuchoka ninakozungumzia si kule kwa kufanya kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kuuza duka, kuwa bize na watoto, hapana!
Shoga kilichonisukuma leo kuandika haya ni mahususi kwa wenzetu walee ambao huwanyima waume zao chakula cha usiku, najua nikisema chakula cha usiku umenipata shoga yangu, kama hujanipata basi hapa patakuwa hapakuhusu, upo? Shoga hivi ujue kuna wanawake wana kauli za ajabu kwa waume zao hasa ukifika muda wetu ule wa chakula cha usiku.

Utasikia anadai kwamba amechoka hivyo ahitaji kusumbuliwa, looo! Aibu! Ngoja niwaulize, hivi unapomwambia mumeo kwamba umechoka na huwezi kumpa chakula cha usiku unafikiri nani atakayempa chakula hicho?
Shoga, nafikiri unajua mtu anapokuwa na njaa anahitaji nini ili hali yake iwe sawa, ni wazi kwamba anahitaji chakula, akila utamuona anavyochangamka kwa furaha, umeona enhh!
Hiyo ni njaa ya kawaida, sasa inakuwaje kwa yule mwanaume mwenye hamu ya mambo yetu yalee, anayekuwa amemmisi sana mkewe na kuhitaji kupata naye chakula cha usiku halafu mkewe amwambie amechoka na hajisikii.
Bila shaka, atanyong’onyea na ni rahisi kuamua kuitafuta shibe hiyo kwa wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula hicho bila masharti tena kikienda sambamba na mapochopocho kibao, umenipata shoga!
Wakati mwingine sikatai, inawezekana ni kweli kuwa umechoshwa na majukumu ya nyumbani au ofisini, lakini ni vyema kutumia lugha ya kujiongeza kumuelewesha mumeo ili akuelewe kuliko kumwambia;
“Na wewe baba Jamal umezidi, kila siku unataka, nimekwambia nimechoka, sitaki sasa!” Shoga kuna wengine wanadiriki kuwaambia kwamba kama wamebanwa sana na njaa wakatafute wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula cha usiku kila siku.Shoga yangu, hivi unaipenda ndoa yako kweli?
Hujui kama kauli za namna hiyo zinaweza kuisambaratisha ndoa yako na mumeo kuamua kutafuta mtu mwingine mwenye kauli nzuri za kujitetea inapotokea amechoka na mumewe kuhitaji chakula cha usiku. Shoga nina mengi ya kuzungumza na wewe lakini kwa leo niishie hapa.
Tukutane tena Jumanne ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi!
GPL

1 comment:

  1. Hivi kweli umeona kabisa hilo ndio jambo litakalo dumusha mahusiano? Je inamaana mwanamke yeye mahitaji yake yanatimizwa kikamilifu na huyo mwanaume au ya kwakwe sio ya muhimu. Na kama uliyeandika hii habari ni mwanamke naomba usizidi kupotosha jamii na watoto wa kike kwa mitazamo yako finyo. Wanawake ni watu wanaotakatikiwa kusimama kutumia mda wao kujiendeleza na sio kuwaza tu nitamridhishaje mwanaume ambaye mwisho wa siku hamna tofauti, MATATIZO YOTE HUKU DUNIANI yanatokana na wanaume ambao wako so selfish na kufikiri mwanamke ni second class citizen. Hata pakujifungulia hakuna,dawa hakuna, heshima ndio usiseme na kupigwa juu hat akuuwawa badala uwashauri wanawake wajuwe kujikomboa unasema watoe chakula cha usiku ...tena wafe njaa kabisa, hakuna mtu kula mchana wala subuhi kwasababu hakuna anayestahili. Kila siku ma vita tu, umeona rahisi wa marekani akimjali hata mkewe..wanaume wachache sana kama Obama ndio wanajua hilo na lazima mwanamke usimame na kupambana na maisha sio kujilekeza na kutaka mwanaume akupe hiki na kile unless wewe sio kilema. Wanawake ni watu wa kuheshimu na wao ndio wataanza kujiheshimu wenyewe kwa kusimama kwa miguu yako najasho lako na kujitoa kwenye utumwa ....If YOU SHE IS TIRED YES SHE IS, YEYE SIO DONKEY...UMEONA MWANAUME MBONA MWANAUME AKICHOKA HATAKI KUSUMBULIWA.... PLEASE ...JUST STOP CANT TAKE THIS NONSENSE...MIND YOU, YOU ARE SHAPING THE YOUNG MINDS...

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake