Wednesday, January 25, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWASILI MKOA WA SONGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA IDARA ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi na kutembelea idara zilizopo chini ya wizara yake kwa lengo la kufuatilia utendaji kazi wa idara hizo na kuzishauri.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Mathias Nyange(kulia), akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kutembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi mkoani Songwe wakati wa ziara ya naibu waziri yenye lengo la kufuatilia utendaji kazi wa idara za wizara yake  na kuzishauri ili kuweza kudhibiti hali ya uhalifu mkoani hapo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakuu wa Idara zilizopo chini ya wizara yake, alipowasili mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi ikiwepo kufuatilia utendaji wa idara hizo katika kukabiliana na hali ya usalama kwa mikoa iliyopo mipakani.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Songwe, Coletha Peter, alipofanya ziara katika ofisi hizo kwa lengo la kujua zoezi la kuandikisha wafanyakazi wa umma lilipofikia.
 Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  baada ya kupata maelezo ya mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe unaojengwa kwa ushrikiano wa wadau wa mkoa huo na jeshi la polisi.Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ACP Mathias Nyange.
Naibu Waziri wa Wizara ya   Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa idara zilizopo chini ya wizara yake katika mkoa wa Songwe  mara baada ya kufanya mazungumzo na wafungwa katika gereza la wilaya ya Mbozi ambapo aliwataka kufanya kazi wanazopangiwa ili wawe rasilimali watu katika dhana ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake