ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 27, 2017

Mbowe atembelea shamba lake lililopigwa marufuku na Serikali



Mbowe akiwa shambani kwake leo wilayani Hai
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Hai. Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.

Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.

Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.

1 comment:

Anonymous said...

Kweli kama ni kuandama watu kisiasa sasa imevuka mipaka! Tanzania haitaweza kujengwa kwa chuki za kisiasa kamwe. Hiki ni kilimo kinachonufaisha wengi bila kujali itikadi wala dini! Kuzuia kilimo huku tukidai Serikali haina chakula ni aibu. Mtoa tamko.hili kama umetumwa kutoka juu nalo.ni vyema ulitizame kwa jicho la pili na kutoa ushauri. Baadae tutasikia polisinwanatumwa kufukuza wahudumu na kuharibu huu ni unyama!!Viongozi wetu tujitizame kwa kumshauri mtoa amri!