Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) ramani ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule.Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Utengule baada ya kuzindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika
kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.Naibu Waziri aliwashukuru wananchi hao kwa
kujitolea eneo la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa jeshi ikiwa ni
juhudi zao katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment