Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Serikali
imekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kuboresha mitaala yake ili
kuendana na mageuzi makubwa yanayofanywa katika sekta ya uchukuzi hapa nchini.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo katika
mahafali ya 32 ya Chuo hicho na kusisitiza kuwa Serikali itatoa nyenzo zote
stahiki kwa chuo hicho ili kukiwezesha kutoa wanafunzi watakaokuwa na soko
ndani na nje ya nchi.
“Tumeanza
kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Uchukuzi ambapo tayari tumenunua ndege
katika mkakati wa kuboresha usafiri wa anga na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa
reli ya kisasa (standard gauge), itakayowezesha treni ya kisasa naya mwendo
kasi kutoa huduma kwa kuanzia Dar es salaam hadi Morogoro”, amesema Waziri
Prof. Mbarawa.
Amesema reli ya
kisasa itakuwa inatumia umeme ili kuwa na mwendo kasi wa kilomita 160 kwa saa
na hivyo kuwezesha usafiri wa Dar es Salaam-Morogoro kuwa wa chini ya muda wa
saa mbili.
Amesisitiza awamu
ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo utaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu
za kumpata mzabuni wa ujenzi huo kukamilika.
Amebainisha
kuwa katika mwaka wa fedha ujao, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya
kukarabati ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho ili kukiwezesha kuwa cha kisasa
na kitakachotoa elimu bora katika ukanda wa Kusini mwa Afrika na kuhakikisha
wahitimu wa fani ya ‘Logistics na
Transport Management’ wanapata bodi ya kitaaluma ili kuratibu fani hiyo .
“Hakikisheni
mnaimarisha utawala bora, utafiti, ushauri wa kitaalamu, machapisho na huduma
yenu iwe ya viwango vya ubora ili kuwezesha wahitimu wenu kupata soko pindi
wanapohitimu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa
amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kwa juhudi, bidii na maarifa
ili kuleta manufaa kwao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Blasius Nyichomba amewataka wahitimu
kuendela kujifunza wawapo sehemu za kazi ili wawe watendaji bora na kujiepusha
na majanga ya utumiaji wa madawa ya
kulevya, ulevi na ukimwi ambavyo vina athiri wataalamu wengi hapa nchini.
Ameongeza kuwa
Chuo hicho kina mpango wa kuanzisha mfumo wa uatamiaji wanafunzi ili kuwawesha
wahitimu kupata ajira mara wamalizapo masomo yao.
Kwa upande wake
Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa amesema idadi ya Wanafunzi katika
chuo hicho imeongeza kutoka 3500 mwaka 2014/15 hadi kufikia 5340 mwaka huu na
wahadhiri wameongezeka kutoka 63 mwaka 2012 hadi 167 mwaka 2017.
Zaidi ya
wanafunzi 1,029 wamehitimu Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada
na Diploma katika fani mbalimbali za usafirishaji na menejimenti zitolewazo
katika Chuo hicho.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba za Viongozi mbalimbali wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Wafanyakazi wa chuoni hapo mara baada ya mahafali yaliyofanyika leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
No comments:
Post a Comment