ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 13, 2017

DK.SHEIN AWASIRI ZANZIBAR AKITOKEA DODOMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini Christina Mndeme (kushoto) pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma leo baada ya kumalizika kwa Vikao vya Chama cha CCM Ukiwemo Mkutano Mkuu maalum uliofanyika juzi katika ukumbi wa mpya wa Kiwete Hall uliopo nje ya Mji wa Dodoma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine  waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu malaaum uliofanyika juzi.(Picha na Ikulu)

No comments: