ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 15, 2017

PITA PITA YA UKODAK WA VIJIMAMBOBLOG SHULE YA MSINGI ALIE SOMA MH. RIDHIWANI KIKWETE

Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa kuchaguliwa wa Chalinze alianza shule ya msingi mwaka 1987 pale shule ya msingi MATANGINI,Nachingwea mkoa wa LINDI. Sababu kubwa za yeye kuanza shule hapa ni kazi aliyokuwa,

 akifanya baba yake kipindi hicho. ikumbukwe kuwa bwana Kikwete alikuwa katibu wa CCM ,wilayani hapo. mwaka mmoja baadae, bwana Ridhiwani na baba yake waliamia MASASI,mkoa wa MTWARA.akiwa huko alijiunga na shule ya MKOMAINDO kwa masomo yake ya darasa la pili kabla hawajarudi DAR ES SAALAAM, mwaka1989 ambapo alijiunga na shule ya FORODHANI iliyopo maeneo ya posta ya zamani hadi alipomaliza darasa la saba.

masomo ya sekondari aliyapata katika shule ya SHAABAN ROBERT na baadae MKWAWA mkoani IRINGA kabla ya kurudi DAR ES SALAAAM kwa ajili ya elimu ya juu katika CHUO KIKUUU CHA DAR ES SALAAM, sehemu ya mlimani na baadae ENGLAND,kwa masomo ya cheti cha elimu ya juu.

Devoo Mdudu rafiki wa Ny Ebra akichungulia barabara aliyokuwa anatumia Ridhiwani kupita kuelekea shuleni hapa.

No comments: