Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya kusaidia
wakina mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo mabeseni 100 yenye vifaa hivyo
kati ya 1000 yalikabidhiwa kwa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dar Es
Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya
kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya
wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya
kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsalimia mtoto mwenye miezi miwili Jenifer Mathias, kulia ni baba wa mtoto Bw. Mathias Miano mkazi wa Kingugi, Mbagala kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya
kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Sehemu ya wananchi wa Mbagala Kizuiani kwenye kituo cha Afya cha Mbagala Round Table waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya
kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi
la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait
nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu na
Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es
Salaam.
Lengo la
mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake wajawazito wasio
na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na
vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia
kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito
kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini unaowakabili.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa mabeseni yenye
vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao
baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo
vya afya kwa kukosa vifaa hivyo kwa
sababu ya umaskini.
Amesema
mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea
kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na umuhimu wa sekta ya
afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti ya mwaka 2017/2018.
Makamu wa
Rais ameeleza kuwa mradi huo wa ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba katika mradi
huo kuanzia sasa utasimamia na wake wa viongozi wastaafu na wakiwemo wake wa
mawaziri baada ya kuuzindua rasmi.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada wake
huo ambao amesema utakuwa ni chachu ya kupambana na vifo vya watoto na wanawake
wajawazito Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa upande
wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya Kuwait
kupitia kwa Jumuiya ya Red Crescent ya nchini hiyo itaendelea kusaidia vifaa
tiba mbalimbali kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na maeneo yao.
Balozi huyo
wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesisitiza kuwa milango ya ubalozi wa
Kuwait ipo wazi kwa Taasisi mbalimbali za Kiserikali kupeleka maandiko
mbalimbali kwa ajili ya kuomba kupatiwa misaada lengo likiwa ni kuhakikisha
wananchi wa Tanzania wanapata huduma za viwango vya juu katika sekta
mbalimbali.
Amesema kwa
sasa Serikali ya Kuwait ipo mbioni kutiliana saini ya makubaliano na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa katika hospitali
ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja.
Ameeleza
kuwa ukarabati huo utaiwezesha hospitali hiyo kuongeza utoaji wa huduma bora
kwa wananchi wengi zaidi.
Halfa ya
makabidhiano ya mabeseni 200 ya vifaa tiba katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu
na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es
Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda.
No comments:
Post a Comment