Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.
Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.
Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.
"Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,"
Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.
No comments:
Post a Comment