Mkuu wa Jeshi la polisi Simon Sirro amewataka wananchi kote nchini kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi kufanya kazi kwa ukaribu na Jeshi hilo ili kuhakikisha linawabaini watu wanaojihusisha na vikundi vya kihalifu.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi mwenye dhama ya kuhakikisha raia wa Tanzania na mali zao wanakuwa salama amesema ili kuimarisha ulinzi zaidi wa Raia vikundi vya ulinzi shirikishi ni muhimu.
Amesema hayo punde kabla ya kukabidhiwa magari manne na kampuni ya kichina ya Great Wall,na kusema kuwa vikundi vya kiharifu vilivyojificha Kibiti siku zao zinahesabika.
Awali Kamishina na Utawala na fedha Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi Kamishina Albart Nyamhanga amesema msaada huo umeokoa fedha ambazo zingetumika kununua magari kama hayo na sasa fedha hizo zitaelekezwa katika matumizi mengine.
Chanzo: ITV Tanzania
No comments:
Post a Comment