Advertisements

Tuesday, July 25, 2017

MASANJA AWAJULIA HALI WATOTO WALIOPATA AJALI

Masanja Mkandamizaji akiwa na watoto Sadia na Wilson majeruhi wa Lucky Vincent wanaotibiwa nchini Marekani.
Masanja akiwa na mtoto Sadia
akiwa na watoto hao, wazazi na ndugu zao.
Wote wakifurahi kwa pamoja.

MMOJA wa wasanii wa vichekesho waliokuwa wakiunda kundi la Orijino Komedi ambaye kwa sasa ni mchungaji, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji, amewatembelea watoto Sadia na Wilson walioko Marekani kwa ajili ya matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masanja Mkandamizaji ameposti picha akiwa na watoto hao na kuandika ujumbe ufuatao.

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu….. Imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja.

Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha safari ya wao kuja Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri!!
Shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea,
wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.”

Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.

Pia majeruhi hao wanatarajia kurejea nchini Agosti 18, Ijumaa saa 3 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na afya zao kuimarika.

Na Isri Mohamed/GPL

No comments: