Advertisements

Sunday, July 23, 2017

NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO ATEMBELEA SHULE YA WATOTO MAHITAJI MAALUM YA BUHAGIJA MKOANI SHINYANGA.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla (Mb) akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Shule ya Watoto wenye mahitaji Maalum ya Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhangija wakiingia kwa wimbo wa kumakribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) alipofanya ziara katika Shule ya Watoto wenye mahitaji Maalum ya Buhagija iliyopo mkoani Shinyanga.
 Mmoja wa mwanafunzi anayesoma katika Shule ya watoto wenye mahitaji Maalum Buhangija Peter Berias Magoti akitoa shukrani zake kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) kwa niaba ya Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya shule hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb)akimpongeza mwanafunzi Peter Berias Magoti  mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya watoto wenye mahitaji Maalum Buhangija.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akitoa pongezi mara baada ya kupokea machapisho kutoka kwa Bi Vicky Mtetema mkurugenzi wa Bodi ya Under the Same Sun wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara katika Shule ya watoto wenye mahitaji Maalum Buhangija, mkoani Shinyanga.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Nyabanganga Taraba akizungumza na familia ya Buhangija alipofanya ziara katika Shule ya watoto wenye mahitaji Maalum Buhangija wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) alitembelea Shule hiyo ya watoto wenye mahitaji Maalum na kufanya kikao na watoto Buhangija. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhagija  mkoani Shinyanga wakati alipofanya ziara katika Shule hiyo mapema wiki hii.
 Baadhi ya wadau wa watoto wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb), (Huyupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara katika Shule hiyo ya watoto wenye mahitaji Maalum Buhangija, Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa mkoa na wilaya ya Shinyanga, Wizara na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija mkoani Shinyanga.

Picha na Erasto Ching’oro WAMJW

No comments: