Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Camosun nchini Canada, Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika.
Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa kozi ya ufundi bomba, mafuta na gesi uliozinduliwa katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC).
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa
uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada
kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.
Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na
aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye
utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo
imenekana kuna pengo kubwa nchini.
"Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata
wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa
kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,"alisema
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk
Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu
wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda
mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.
Alisema kozi hiyo ni nyumbufu
itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa
kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa
maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.
Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo
ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema
wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii
kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.
No comments:
Post a Comment